SHAMBA LA KUKU
Ni kitabu Cha Tiba na mbinu za ufugaji Bora.
Kimejumuisha ufugaji wa kuku, Bata, kanga , Njiwa na kware.
Kitabu hiki ni suluhisho kwa wadau ambao hawajawahi kufuga, au wanafuga na wanahitaji kuongeza maarifa ili kuleta tija kwenye ufugaji wao.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili ili kieleweke kwa urahisi na walengwa ambao ni wafugaji, maafsa mifugo, madaktari wa wanyama, pamoja na wadau wengine ambao wanataraji kuanza ufugaji, kwa matokeo bora na endelevu.
Kupitia kitabu hiki utajifunza:
1)Njia bora za uleaji wa vifaranga wa kuku aina zote, bata , kanga, njiwa na kware.
2)Ujenzi wa mabanda, vipimo na uwiano shambani(layout).
3)Magonjwa ya kuku, bata, kanga, njiwa na kware, pamoja na dalili na tiba zake.
4)Namna ya kuweka biosecurity shambani(usalama wa mazingira kuepuka milipuko ya magonjwa).
5)Utoaji wa chanjo na kalenda zake.
6)Uchanganyaji wa vyakula, kupata chakula cha vifafanga(starter), chakula cha kuku wanaokuwa(growers), chakula cha kuku wanaotaga(layers feed), chakula cha kumalizia/kunenepesha(Finisher).
7)N.k
Gharama ya kitabu hiki ni Tsh. 10,000/= Hard copy, wasiliana nasi kupata Nakala mahala popote ulipo, Tanzania.